Jumatatu 14 Septemba 2026 - 01:39
Kupokea Posho na Msaada wa Kifedha Pasi na Kuzingatia Ratiba ya Masomo

Hawzah/ Ayatullah Shahidi Sayyid Ali Khamenei amejibu swali la kisheria kuhusu “kupokea posho ya masomo na msaada wa kifedha pasi na kuzingatia ratiba ya masomo.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Shahidi Sayyid Ali Khamenei amejibu swali la kisheria kuhusu “kupokea posho ya masomo na msaada wa kifedha pasi na kuzingatia ratiba ya masomo,” swali ambalo linawasilishwa kwa wasomaji na wale wanaopenda kufahamu hukumu hii kama ifuatavyo:

Uzembe Katika Kutafuta Elimu na Kupoteza Muda

Swali:
Ni ipi hukumu ya wanafunzi wa shule, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafunzi wote wanaosoma taaluma mbalimbali, kuhusu kupokea posho ya masomo na msaada wa kifedha bila kuzingatia ratiba ya masomo?

Jawabu:
Wanafunzi wa shule, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafunzi wote wanaosoma taaluma mbalimbali, muda wa kuwa wananufaika na huduma na marupurupu ya shule au chuo husika, wanapaswa kufuata ratiba ya masomo ya taasisi hiyo. Vinginevyo, kujinufaisha kwao na posho ya masomo, msaada wa kifedha na marupurupu mengine ni haramu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha